Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Bi. Pendo Mahalu ameishukuru Mamlaka ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kutoa msaada wa vifaa tiba pamoja na fedha taslimu Tsh Mil 10 ambazo zimetolewa kwajili ya ujenzi wa Uzio kwenye eneo la Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni (KDH) pamoja na kuboresha utoaji wa huduma ya Afya Hospitali hapo.
Bi. Pendo Mahalu ametoa shukrani hizo leo Septemba 15. 2023 katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye uwanja wa Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni ambapo alipokea msaada huo kwa niamba ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo.
" Sisi kama kama Wilaya kwakweli tunaishukuru Mamlaka ya Bandari ya Dar es Salaam kwa msaada ambao wametoa na tunaahidi fedha hizi zitakwenda kufanya lengo ambalo limekusudiwa likiwa ni la kujenga uzio, pia vifaa tiba vitakwenda kutumiwa na wagonjwa au wahitaji ambao watakuja kupata huduma katika Hospitali zetu." Alisema
Sambamba na hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Dar es Salaam Ndugu Mrisho Selemani Mrisho amesema wametoa msaada huo ikiwa ni maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa Mamalaka ya Bandari Tanzania
Pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuboresha Badari ya Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza mapato ya bandari na Taifa kwa ujumla.
Aidha amesema Mamlaka ya Bandari ya Dar es Salaam itaendelea kushirikiana na jamii kwa la kuboresha huduma mbalimbali katika sekta ya Afya pamoja na Elimu.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Erasto Kiwale ameishukuru Mamlaka hiyo na amewaomba kuendelea kutoa Msaada kwa kuangalia Sekta nyingine hususani katika elimu ambapo miundombinu bado inahitaji kuboreshwa.
Hafla hiyo ilihitimishwa kwa zoezi la upandaji wa Miti Hspitalini hapo ambapo jumla ya miti 200 ilipandwa.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa