" *Kumekuwa na tabia ya baadhi ya Viongozi kuuza maeneo yasiyo rasmi na pia wananchi wenyewe kuvamia maeneo yasiyo rasmi kama mabondeni na kwenda kufanya shughuli mbalimbali, maeneo ya open space, maeneo ya makaburi na hata maeneo ya mashuleni na wengine kwenda kujenga kabisa nyumba zao za makazi, niwaambie hilo ni kosa kisheria na hatutamvumilia yeyote anayejihusisha na suala hilo na tukikubaini tutakuchukulia hatua za kisheria* "
" *Natoa agizo kwenu wote mliovamia maeneo yasiyo rasmi kuondoka mara moja na nitoe rai kwenu wananchi kuwa Mabalozi katika hili na tumeanza kuchukua hatua kwa kuwaandikia barua wale wote waliovamia maeneo hayo kuondoka mara moja* "
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya mtaa kwa mtaa ambapo leo tarehe 4 Julai, 2023 amefika katika mtaa wa Kichangani, Sokoni na Uvumba katika Kata ya Kibada.
DC Bulembo pia ametoa rai kwa wananchi kushiriki mazoezi ya usafi wa pamoja kwa maslai ya kutunza mazingira " *Tunakuja na sheria ndogondogo zitakazomuamrisha kila mwananachi kufanya usafi eneo la pembenne za mazingira anayoishi, lazima mfanye usafi tutunze mazingira yetu na hii ni Ajenda ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam lazima itekelezwe, tunakuja mara nyingi kwenye mazoezi ya usafi lakini hamjitokezi, rai yangu kwenu ni kujitokeza na kufanya usafi na tutunze vyanzo vya maji na kupanda miti* " Alisema DC Bulembo.
Katika hatua nyingine, DC Bulembo ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Afisa Michezo Manispaa ya Kigamboni hadi kufikia tarehe 6 mwezi Agosti kiwanja cha michezo cha kibada kiwe kimerekebishwa ili kuwezesha Vijana kutumia kwa michezo kwani michezo ni Afya na ni Ajira.
Naye Kaimu Mkurugenzi Bw. Juvenaris Mauna ametoa wito kwa Wananchi na Viongozi wa Serikali za mitaa kutobadilisha matumizi ya maeneo yaliyotengwa kwa huduma za kijamii kiholela.
Katika kujibu kero mbalimbali za wananchi, Meneja TANESCO amesema ndani ya miezi 2 huduma ya umeme itakuwa imefika maeneo yote ya block D Kibada na sasa nguzo zimeshaanza kupelekwa hadi maeneo ya Block 5.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa