Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almasi Nyangassa amewashukuru NMB kwa msaada wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya M.25 walivyotoa katika Hospitali ya Wilaya ( mabenchi 50 ya kupumzikia wagonjwa) , Madawati 50 shule ya msingi Ungindoni , mabati 200 Shule ya Msingi Rahaleo na mabati 180 Sekondari ya Kigamboni ikiwa ni sehemu ya kurejesha faida kwa jamii.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya amesema vifaa walivyovitoa vitasaidia kuboresha utoaji huduma na kitendo cha NMB kuichagua Kigamboni kimeonesha ushirikiano mzuri walionao kwani wangeweza kwenda kwingine sababu wahitaji ni wengi.
Ameongeza kwa kusema kuwa changamoto haziishi lakini tunaowajibu wa kuhakikisha tunatatua moja moja kwa kadri nafasi inapopatikana hivyo, amewaomba NMB kuendelea kuishika mkono Kigamboni katika kusaidia juhudi za Serikali za kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Wakati huohuo amewataka wahudumu wa afya na walimu wa shule waliopokea vifaa kuhakikisha wanavitunza na kutumia kadri ya mahitaji ili kuwapa morali NMB na wadau wengine kuendelea kuiona Kigamboni inastahili kupewa kipaumbele katika kuunga mkono juhudi za maendeleo.
Mstahiki Meya wa Manispaa Mhe. Ernest Mafimbo amewashukuru NMB kwa niaba ya wananchi na kusema kuwa Serikali haina uwezo wa kutatua changamoto zote kulingana na ufinyu wa bajeti hivyo wanapotokea wadau kama NMB inakuwa inaisaidia katika utoaji huduma bora.
Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam Donatus Richard ameishukuru kigamboni kwa ushirikiano na kuwatambua kama wadau wa maendeleo na kusema kuwa kila mwaka imekua ikitenga 1% kwaajili ya kurudisha faida kwa jamii na wamelenga maeneo ya afya, elimu na majanga yasiyotegemewa.
Ameongeza kuwa kwa mwaka uliopita walitenga zaidi ya Bilioni 2 ili itumike katika kurejesha kwa jamii , kigamboni ni jamii yao na wamekuja kuadhimisha rejesho kwa jamii kwani hawawezi kuendelea kama jamii haipo.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Fatma Almasi Nyangassa akiwashukuru NMB kwa kuamua kuifanya Kigamboni kuwa sehemu ya upokeaji wa faida kwa jamii.
Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam Donatus Richard na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almasi Nyangassa wakizungumza wakati wa makabidhiano ya madawati ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ungindoni.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almasi Nyangassa akielezea namna mabenchi yaliyotolewa yataziba nafasi zilizokuwa zinawafanya wagonjwa kusimama wakingoja huduma.
Viongozi wakiwa kwenye picha ya pamoja Mara baada ya kukabidhiana mabenchi ya kuketia wagonjwa pindi wanaposubiri huduma
Mstahiki Meya Manispaa ya Kigamboni Mhe.Ernest Mafimbo akishukuru NMB kwa niaba ya wananchi kwa msaada wa vifaa walivyovikabidhi.
Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam Donatus Richard akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa ikiwa sehemu yao ya kurejesha faida kwa jamii.
Baadhi ya madawati yaliyotolewa.
Mkuu wa Wilaya Mhe.Fatma Almas Nyangassa kulia na Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam Donatus Richard wakikabidhiana mabenchi ya kupumzikia wagonjwa wakati wanangoja huduma.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa