Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh. Halima Bulembo ameendelea na ziara yake ya Mtaa kwa mtaa ikiwa leo ametembelea Mtaa wa Puna, kibungo, mahenge na kwa Morisi katika kata ya Pembamnazi.
Akizungumza mara baada ya kuwasili katika ziara Mh. Bulembo amemtaka Afisa Biashara kuhakikisha anatengeneza mazingira rafiki yatakayo wavutia wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika ardhi ya wilaya Kigamboni huku akiwasisitiza wawekezaji kutoa ajira kwa wananchi wa kigamboni kabla ya kufikiria kuajiri wakazi wa wilaya za jirani.
Sambamba na hilo Mh. Bulembo alitoa onyo kwa vijana wa kigamboni kufanya kazi kwa weledi na kuacha tabia zisizofaa zinazoweza kuwafanya washindwe kuaminika na hatimae kupoteza sifa za kupata ajira toka kwa wawekezaji.
Akizungumzia changamoto ya maji inayowakabili wakazi wa pemba mnazi Mh. Bulembo kupitia Meneja wa DAwasa amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 inayotarajiwa kuanza Julai mwaka huu tayari takribani km 50 zimeshapangiwa kusambazwa mabomba ya maji na wastani wa km 20 zitafika kwenye mitaa iliyopo kata ya pemba mnazi na kazi hiyo inatarajiwa kuanza mara baada ya bajeti kupita.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa