Kata hii ipo kaskazini mashariki ya wilaya ya Kigamboni. Kaskazini imepakana na kata ya Tungi, Mashariki imepakana na Bahari ya Hindi, Kusini imepakana na na Kata ya Somangira,Magharibi imepakana na kata ya Vijibweni.
Utawala
Kata hii huundwa na Mitaa minne nayo ni Mjimwema, Maweni, Kibugumo, na Ungindoni. Kata hii ndio yenye Ofisi za Mkuu Wilaya kwa sasa.
Idadi ya Watu
Kata ya Mjimwema in jumla ya Wakazi 33,266 Wanaume 16,448 wanawake 16,818
Diwani
Diwani wa kata hii ni Mh.Selestine Prosper Maufi.
Shughuli za kiuchumi
Wakazi wa kata hii hujishughulisha na Uvuvi kwa wale ambao ni wenyeji na biashara ndogondogo. Pia kuna Hoteli za kitalii katika fukwe zake kama vile Sunrise, South Beach.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa