Kata ya Kimbiji imepakana na Bahari ya hindi mashariki Kata ya Somangila Kusini, Magharibi kata ya Kisarawe II, na kaskazini kata ya Pembamnazi Sura ya nchi ya kata hi ni tambarare, ina udongo wa kichanga na tifutifu.
Utawala
Kimbiji inajumuisha mitaa sita ambayo ni Kwachale, Kizito huonjwa, Ngobanya , Mikenge, Kijaka na Golani.Makao makuu ya kata ya kimbiji yapo Kwachale umbali wa takribani kilomita arobaini toka Feri-Kigamboni.
Diwani
Diwani wa kata ya Kimbiji ni Mh.Samiya Muhidini Ruhaya.
Shughuli za kiuchumi
Wakazi wa kata hii hujishughulisha zaidi na shughuli za kilimo cha mpunga, matikiti, muhogo, mbogamboga na Uvuvi. Pia kuna kiwanda cha cement cha Lake katika Kata hii. Kimbiji ni Kata ambayo ina fukwe nyingi nakufanya hoteli nyingi za kitalii kujengwa pembezoni mwa eneo hili.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa