Utaratibu wa utoaji wa miliki
1.Mahitaji ya umilikishaji wa miliki mhusika/mwombaji miliki anatakiwa awe na vitu vifuatavyo:
• Ramani ya eneo husika.
• Uthibitisho wa Uraia.
• Mkataba wa mauziano/uthibitisho toka kwa mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kama alimilikishwa kienyeji.
• Aandike barua ya maombi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ikipitia kwa Afisa Mtendaji wa Kata kilipo kiwanja hicho na kwa mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo.
• Muombaji/mhusika atajaza Form No. 19.
2. UMILIKISHWAJI
(A) Umilikishwaji wa “Allocation Letter” (miliki).
Utaratibu wa kuandaliwa “Allocation Letter unafuata baada ya mhitaji kukamilisha mahitaji yote ya umilikishwaji. Utaratibu huo ni:-
• Kufungulishwa file la kiwanja hicho.
• Matumizi ya kiwanja hicho kutolewa na Afisa Mipango Miji.
• Makadirio ya kodi ya ardhi kuandaliwa na mthamini.
• Maandalizi ya “Allocation Letter” yanakamilishwa.
(B) Utoaji wa Hati miliki
Utoaji wa Hati hufanyika baada ya kuandaliwa “Allocation Letter”. Iwapo hakutakuwa na allocation letter hati haiwezi kuandaliwa. Utaratibu wa kuandaa hati ni kama ifuatavyo:
• Ushuhuda wa malipo ambayo huandaliwa baada ya mhitaji/mmiliki kulipia ada za Serikali zilizoainishwa kwenye “Allocation Letter”.
• Maombi ya ramani na maandalizi ya ramani hufanyika (Request for Deed Plan).
• Mpima huandaa Ramani za Hati na kuzipitisha .
• Maandalizi ya Hati miliki yanafanyika.
• Mhusika anasaini Hati miliki kwa kushuhudiwa na wakili au Mwanasheria.
• Maafisa Ardhi Huandaa Historia ya kiwanja hicho, na kupeleka kwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya
saini na usajili.
• Mhusika hufuata Hati yake kwa msajili wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa