Saturday 2nd, December 2023
@Kila Kaya
SANSA YA WATU NA MAKAZI
SENSA NI NINI?
Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchakata, kuchambua na kusambaza taarifa za kidemografia, kiuchumi, mazingira na kijamii za watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum.
HISTORIA YA SENSA KIGAMBONI
Kwa mujibu wa sensa ya Mwaka 2002, idadi ya watu ilikuwa 36,701, Mwaka 2012 idadi ya watu ilikuwa 162,932. Hadi kufikia Juni, 30 Mwaka 2021 idadi ya watu kwa Wilaya ya Kigamboni inakadiriwa kuwa 267,934 sawa na ongezeko la asilimia 60.8.
UMUHIMU WA SENSA YA WATU NA MAKAZI
.Kuboresha miundombinu ya huduma za jamii (afya, elimu, maji, , umeme n.k).
.Kurahisisha mipango mbalimbali ya maendeleo.
.Kusaidia katika tafiti mbalimbali kwenye jamii.
.Kutambua mahitaji ya jamii.
KWANINI MTU WA KAWAIDA AKUBALI KUHESABIWA?
Kukataa kuhesabiwa ni kujinyima haki fungu lako katika Mipango ya Maendeleo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa