Manispaa ya Kigamboni ni miongoni mwa Wilaya ambayo Kilimo huchangia katika kuongeza kipato kwa wakazi, upatikanaji wa chakula (lishe bora) na hifadhi ya mazingira. baadhi ya mazao ya kilimo yanayotumiwa na wakazi wa Jiji huzalishwa katika maeneo mbalimbali katikati na pembezoni mwa Wilaya. Mboga za majani na matunda ni mazao muhimu yanayozalishwa kutokana na kuwa karibu na soko (walaji) na bei nzuri. Mboga zinazozalishwa ni mchicha, matembele, chainizi kabichi, bamia, kisamvu, sukuma wiki, bilinganya, uyoga, mnavu, kisamvu na maboga. Matunda ni pamoja na makakara, matango, papai, nanasi, matikiti maji, na machungwa.
Fursa zilizoko katika Kilimo
Wilaya ina fursa nyingi katika kilimo kutokana na kuwa karibu na soko kubwa (walaji), na kuwa na makampuni ya usindikaji na miundombinu mizuri ya usafirishaji wa bidhaa ndani ni mkoa na nje ya Mkoa. Mkoa una makampuni makubwa na madogo ya usindikaji wa mazao ya kilimo kama vile matunda, nafaka, hivyo hufanya kilimo kuwa na fursa nzuri katika wilaya.
Wilaya ya Kigamboni kuwa moja ya wilaya za jiji la Dar es salaam, kumefanya wilaya kuwa na fursa nzuri ya kilimo cha mazao mbalimbali, kwani Takwimu zinaonesha kuwa kaya za jiji la Dar es Salaam zina kiwango kidogo cha umaskini wa mahitaji ya msingi ukilinganisha na kaya zinazoishi katika miji mingine na maeneo ya vijijini. Hii ni fursa kwa wazalishaji, wataalam wa ugani, wawekezaji na wadau mbalimbali wa kilimo kuongeza thamani katika bidhaa za kilimo na kuzingatia ubora katika uzalishaji, hususani matumizi ya kilimo hai (organic agriculture) ili kuchangamkia fursa hii inayoongezeka kwa kasi kutokana na kukua kwa kipato na uelewa wa wakazi wa Dar es Salaam.
Mazao kama vile korosho, muhogo na viazi huzalishwa kwa wingi katika Manispaa ya Kigamboni. Usindikaji wa unga wa muhogo na korosho hufanywa kupitia vikundi vilivyopo katika Manispaa. Uwepo wa Bandari ya Dar es Salaam, barabara zinazokwenda mataifa jirani, Mamlaka za Serikali kama vile Wizara mbalimbali za Kisekta ni fursa ambazo zinaweza kutumiwa na wazalishaji, wasindikaji na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo katika kuzalisha, kusindika na kusafirisha bidhaa za kilimo nje ya nchi na kujipatia fedha za kigeni kwa ustawi wa taifa letu.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa