• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Care Values
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu ya awali na Msingi
      • Kilima mifugo na umwagiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Sekondary
      • Mipango na uratibu
      • Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda biashara na Uwekezaji
      • Miundombinu ,Vijijini na Mjini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa jamii na Lishe
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
        • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa ndani
      • Usimamazi wa Manunuzi
      • Maliasili na uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na uhasibu
      • Usimamizi na usafi wa Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Utumishi
    • Huhuma za Kisheria
    • Usafi wa mazingira na udhibiti wa taka ngumu
    • Michezo na Sanaa
  • Madiwani
    • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
      • Huduma za jamii
    • Ratiba za Vikao
      • Vikao vya Waheshimiwa
      • Kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
      • Miradi ya Sasa
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Picha
    • Hotuba
    • Gazeti la Mtandaoni
    • Vipeperushi
  • Mifumo

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.

27 July 2017


Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imepokea kibali Kumb. Na. FA 170/374/01/27 cha tarehe 14 Julai, 2017 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Kibali Kumb. Na. FA.102/282/02B/13 cha tarehe 30 Juni, 2017 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni anawatangazia wananchi wote raia wa Tanzania wenye sifa kuomba nafasi zilizoorodheshwa hapo chini.

  • MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III-  (NAFASI 31)
  • Sifa za Mwombaji
  • Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Kazi na majukumu ya Mtendaji wa Mtaa

  • Katibu wa kamati ya Mtaa
  • Mtendaji Mkuu wa Mtaa
  • Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa
  • Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa
  • Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa
  • Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama
  • Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umaskini katika Mtaa
  • Kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote
  • Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
  •        Ngazi ya mshahara ni TGS B sawa na Shilingi 390,000/= kwa mwezi
  • MTUNZA KUMBUKUMBU MSAIDIZI DARAJA LA II  (NAFASI 5)
  • Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) waliohudhuria mafunzo ya Utunzaji wa Kumbukumbu nakupata cheti cha NTA LEVEL 5 katika mojawapo ya fani za Afya,Masjala, Mahakama na Ardhi
  •  
  • Kazi na Majukumu
  • Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji
  • Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/ nyaraka
  • Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu
  • Kuweka kumbukumbu (barua,nyaraka n.k) katika mafaili
  • Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali
  •           Ngazi ya mshahara ni TGS B sawa na Shilingi 390,000/= kwa mwezi
  • KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III   (NAFASI 1)
  • Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) waliohudhuria mafunzo ya Uhazili nakupata cheti cha NTA LEVEL 5. Wawe wamefaulu somo la hati mkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya kutumia kompyuta kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali nakupata Cheti katika programu za Windows,Microsoft Office,Internet,E-mail na Publisher.
  •  

     KAZI NA MAJUKUMU YA KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III   

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
  • Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
  • Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba za kazi nyingine zilizopangwa kutekelezwa katika Ofisi anayofanyia kazi na kumuarifu mkuu wake kwa wakati unaohitajika
  • Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za hapo Ofisini
  • Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao
  • Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika Sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika
  • Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi
  •     Ngazi ya mshahara ni TGS B sawa na Shilingi 390,000/= kwa mwezi

 

  • MSAIDIZI WA HESABU     (NAFASI 2)

Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotambuliwa na NBAA, waombaji wawe na uzoefu wa kazi zaidi ya mwaka (1) katika fani hiyo

  KAZI NA MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA HESABU.

  • Kuandika na kutunza “register”zinazohusu shughuli za uhasibu
  • Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha
  • Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu
  • Kupeleka barua/ nyaraka za Uhasibu benki Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.
  • Ngazi ya mshahara ni TGS B sawa na Shilingi 390,000/= kwa mwezi

NB. Kwa nafasi ya Msaidizi wa Hesabu itakuwa ni kwa Mkataba wa Mwaka mmoja na waombaji wawe tayari kufanya kazi katika Vituo vya Afya.

  1. MASHARTI KWA UJUMLA
  2. Mwombaji awe raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni
  3. Mwombaji awe na Umri usiozidi miaka 45 na awe hajawahi kupatikana na kosa lolote la jinai, kufungwa jela au kufukuzwa kazi katika Utumishi wa Umma
  4. Waombaji  waambatishe maelezo yao binafsi (C.V)
  5. Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya taaluma, vyeti vya kidato cha (IV au VI), cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi za hivi karibuni na ziandikwe majina nyuma
  6. “Testemonials, provisional results, Statment of Results hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV and FORM VI RESULT SLIPS) HAVITAKUBALIWA
  7. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika TCU na NACTE na taarifa ya uhakiki iambatishwe kwenye maombi
  8. Uwasilishwaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
  9. Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono
  10. Mwisho wa kupokea barua za Maombi ni tarehe 15.08.2017 saa 9:30 alasiri.

 

Maombi yatumwe kwa Anuani ifuatayo:

Mkurugenzi,

Halmashauri ya Manispaa Kigamboni,

S.L.P 36009,

Kigamboni, Dar es Salaam.

 

Matangazo

  • Tangazo la Frem za Biashara, Soko la Kibada February 26, 2025
  • Tangazo la kuitwa kwenye usaili nafasi ya mwendesha mashine ya Bayometriki na Mwandishi msaidizi February 24, 2025
  • Tangazo la uteuzi wa wajumbe wa bodi ya Afya March 26, 2025
  • Tangazo la kuitwa kazini nafasi ya mwendesha mashine ya Bayometriki na Mwandishi msaidizi March 12, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Watumishi wa Manispaa ya Kigamboni watakiwa kutoa huduma bora kwa Wananchi

    June 13, 2025
  • Manispaa ya Kigamboni yatwa Makombe 9 UMITASHUMTA na 15 UMISSETA ngazi ya Mkoa

    June 12, 2025
  • RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE. DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIBADA - MWASONGA

    April 25, 2025
  • MANISPAA YA KIGAMBONI IMEPOKEA VITI MWENDO 35 NYENYE THAMANI YA TSH MIL 8

    April 08, 2025
  • Angalia Zote

Video

Makala maalumu ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Kigamboni
Video zingine

Kurasa za karibu

  • Municipal councilors
  • Kigamboni Municipal History
  • Investment Opportunities
  • Fomu ya Maombi ya Kiwanja
  • Huduma za Afya na Orodha ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni

    Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam

    Simu: +255222928468

    Simu ya Mkononi: +255222928468

    Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa