• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kigamboni Municipal Council
Kigamboni Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Livestock na Fisheries
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Sekondary
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Mipango Mija na Maendeleo ya Ardhi
      • Afya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba za Vikao
      • Vikao vya Waheshimiwa
      • Kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ya Sasa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Picha za Video
    • Hotuba Mbalimbali
    • Picha

“Nimeridhishwa na huduma zinazotolewa na vivuko” DC SARA

Posted on: October 9th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri amesema kuwa ameridhika na hali ya uendeshwaji wa kivuko hususani katika eneo la usalama baada ya kutoa maelekezo kwa wasimamizi wa kivuko kuboresha huduma zinazotolewa hapo.

Mhe. Sara amesema hayo leo alipofanya ziara ya ukaguzi wa utekelazaji wa maagizo aliyoyatoa alipotembelea kivuko hicho mwezi uliopita na kusema kuwa kwa kiwango kikubwa maelekezo yamefanyiwa kazi na mabadiliko makubwa yameonekana.

Aliongeza kuwa wametoa namba za simu za dharula kama alivyoelekeza,  namba ya zimamoto na ukoaji, matangazo yanatolewa yanayoeleza  utaratibu mzima wa kupata huduma za vivuko ikiwemo na uwezo wa vivuko ya ubebaji wa watu na magari, wamefunga luninga kwenye vivuko zinazoonesha video fupifupi za elimu ya uokoaji na mawasiliano kwa watumia vivuko.

“ walau sasa kuna elimu kidogo ya uokozi namna ya kutumia life jacket(vazi la uokoaji), maboya, namna ya kuruka kwenye maji, vifaa vimesafishwa na vimewekwa maeneo ya wazi hakuna kufuli kama zamani kwahiyo likitokea jambo lolote inakuwa rahisi kwa abiria kuvipata kwa haraka, kwa kiasi Fulani nimeridhika bado vitu vichache tu” Amesema Mhe. Sara

Aidha ameelekeza kufungwa kwa luninga  kubwa kwenye maeneo ya kusubiria abiria ili elimu inayotolewa iweze kufikiwa na watumiaji wote wa vivuko,kuweka namba ya simu itakayopigwa bure na mwananchi  ikiwa ni pamoja na kufunga kamera itakayosaidia kufuatilia mwenendo mzima wa huduma zinazotolewa na kivuko.

Akizungumzia suala la wavuvi amesema kuwa ni mtambuka kwasababu jinsi soko lilivyojengwa limelenga wafanyabiashara ambao ni wavuvi, mitumbwi iliyopaki pembezoni ambayo inaingilia njia za meli na vivuko lazima wadau wote wahusike kukaa kwa pamoja na kamati ya ulinzi  na usalama kwasababu hawa wadau wanasheria zinazowaongoza kwa hiyo ni vyema utaratibu ukafuatwa katika kutatua changamoto hiyo.

Mkuu wa Wilaya  pia amepiga marufuku mitumbwi kutumika kuvushia abiria kinyume na taratibu na kusema kwamba sheria zifuatwe kwa yeyote atakayebainika anatumia mitumbwi kuvusha abiria.

Kwa upande wake kaimu mtendaji mkuu wa TEMESA Eng.Japhet Masele ameshukuru na kusema kuwa maagizo mengi ambayo yalikuwa yametolewa yalikuwa yameanza kufanyiwa kazi katika kuboresha huduma za vivuko na kusema kuwa wamejipanga kuwa na usismamizi mkali kipindi cha asubuhi na jioni ambapo kunakuwa na abiria wengi na kueleza kuwa wanahakikisha vivuko vyote nchini vinafanya kazi kwa kuzingatia taratibu na kanuni.

Ameongeza kuwa hivi karibuni  wanaweka mfumo wa kuhesabu(electronic counter)  ili kivuko kinavyopakia uongozi uweze kujua kivuko kimeondoka na ujazo sawa kuepuka kuzidisha uwezo wa kivuko husika.

Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiri akieleza namna alivyoridhishwa na maboresho ya huduma zinazotolewa na vivuko.


baadhi ya abiria wakishuka kwenyhe kivuko baada ya kufika ng'ambo

Mtoa elimu ya kujiokoa kwa kutumia vazi la uokoaji(life jacket) akitoa maelezo ya namna ya kulitumia vazi hilo

elimu ya kutumia boya ikitolewa na mkufunzi wa masuala ya ukoaji

Mkuu wa Wilaya akiwa ameambatana na viongozi wengine wakitoka kwenye kivuko cha Mv Magogoni


Kiongozi wa TEMESA aliyenyoosha mkono akieleza changamoto ya mitumbwi ya wavuvi




moja ya luninga iliyofungwa kwenye kivuko cha Mv Magogoni ikionesha video fupifupi za jinsi ya kujiokoa.

Matangazo

  • Pata matokeo ya kidato cha nne 2018 January 24, 2019
  • Tangazo la orodha ya vibali vya ujenzi vilivyotolewa julai-octoba 2018 November 06, 2018
  • Tangazo la orodha ya vibali vya ujenzi vilivyotolewa tarehe 4 Januari 2019 January 09, 2019
  • Pata matokeo ya darasa la saba mwaka 2018 hapa October 24, 2018
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DC Sara apongeza kamati na uongozi uboreshwaji wa huduma za afya Kigamboni

    February 12, 2019
  • Wananchi wanaoishi mabondeni na maeneo hatarishi watakiwa kuhama

    January 31, 2019
  • Manispaa yatakliwa kubuni vyanzo vya mapato

    January 30, 2019
  • huduma zaidi kuboreshwa kituo cha afya Kigamboni

    January 28, 2019
  • Angalia Zote

Video

Maonesho ya Wakulima na wafugaji
Video zingine

Kurasa za karibu

  • Municipal councilors
  • Kigamboni Municipal History
  • Investment Opportunities
  • Fomu ya Maombi ya Kiwanja
  • Huduma za Afya na Orodha ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Mjimwema Kigamboni

    Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam

    Simu: +255222928468

    Simu ya Mkononi: +255713297256

    Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa