Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo amewataka mama na baba lishe waliopo ndani ya Wilaya ya Kigamboni kujisajili na kupata vitambulisho vya wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga) ili waweze kupata fursa ya mikopo ya 10% inayotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni
Mhe. Bulembo ameyasema hayo leo Februari 16 2034 katika Tamasha la “MAMA LISHE NA SAMIA” lilioandaliwa na Msanii na mjasiliamali Zuwena Mohamed (Shilole) na kufanyika katika viwanja vya Mji Mwem. Manispaa ya Kigamboni.
“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua uwepo na umuhimu wa wajasilimali ndio maana ameidhinisha mikopo ya 10%, Kwa Dar es Salaam ni Kigamboni pekee ndio ina jukwaa la Mama na Baba lishe, hivyo nawasihi elimu mnayoipata hapa ichukueni kwa uzito na mjisajili katika mifumo rasmi ili muweze kuomba mikopo hiyo, taratibu rasmi zipo wazi, nawasihi mfuate utaratibu rasmi ili muweze kupata fedha hizi kwani hii ndiyo fursa ya kujipatia mtaji” amesema Mhe. Halima Bulembo.
Aidha, Mhe. Bulembo amewashukuru waandaaji wa tamasha hilo na kuifanya Kigamboni kuwa Wilaya ya kwanza kufaidika na kampeni hii.
Naye mratibu wa Tamasha hilo Bwn. Amani Martin amesema kuwa lengo la Tamasha hili ni kumshusha Mama na baba lishe kuni kichwani kwa kumuwezesha kiuchumi na kuwapa mitungi ya gesi pamoja na vifaa vingine muhimu ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha wanatumia nishati safi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa