Barabara ya Mikadi Beach - Shelaton yenye jumla ya urefu wa km 1.65 inajengwa kwa awamu, mpaka sasa awamu tatu zenye jumla ya urefu wa km 1.1 zimekamilika na awamu ya nne yenye jumla ya urefu wa km 0.35 inaendelea. Jumla ya gharama ya mradi kwa awamu zote nne ni Sh. 1,931,668,872.50 na jumla ya fedha iliyotumika mpaka sasa kwa awamu zote nne ni Sh.1,403,123,204.00.
Awamu I ya barabara hii ina urefu wa km 0.5 imejengwa katika mwaka wa fedha 2019/2020, kwa chanzo cha fedha kutoka serikali kuu na gharama zilizotumika ni sh. 669,574,400.00. Awamu II ya barabara hii ina urefu wa km 0.3 imejengwa katika mwaka wa fedha 2020/2021 kwa fedha za Mfuko wa Barabara na gharama zilizotumika ni Sh.377,405,054.00. Awamu III ya barabara hii ina urefu wa km 0.3 imejengwa katika mwaka wa fedha 2021/22, kwa chanzo cha fedha kutoka Mfuko wa Barabara na gharama zilizotumika ni sh. 271,633,250.00.
Awamu IV ya ujenzi wa barabara hii ina urefu wa km 0.35 ambayo inajengwa kupitia fedha za Tozo ya nyongeza ya mafuta ya dizeli na petroli, kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22. Mradi huu unajengwa na Mkandarasi Mirogena Investment LTD kwa mkataba Na. AE/092/2021/2022/DSM/W/77 chini ya usimamizi wa ofisi ya TARURA Wilaya ya Kigamboni. Muda wa utekelezaji wa mradi huu ni miezi sita (6), kuanzia tarehe 26/11/2021 na unatarajiwa kukamilika tarehe 26/05/2022. Gharama za mkataba ni Sh. 455,962,710.00, hadi kufikia sasa kiasi cha Sh. 318,965,639.31 kimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji. Mpaka sasa fedha zilizotumika ni Sh. 84,510,500.00.
Ujenzi wa mradi una manufaa yafuatayo; Kupunguza foleni ya vyombo vya usafiri katika eneo la Feri – Kigamboni, Kurahisisha usafiri hasa kipindi cha mvua kwa wananchi wanaofuata huduma mbalimbali za Kijamii, Kupunguza uchakavu wa vyombo vya usafiri, na Inasaidia vyombo vya usafiri kufika kwa wepesi na haraka maeneo ya jiji la Dar es Salaam kupitia daraja la Nyerere. Aidha utekelezaji wa mradi huu umenufaisha wakazi wa eneo husika kupitia mamalishe na vijana kupata ajira za muda mfupi.
Ujenzi awamu ya Tatu.
ujenzi Awamu ya nne
Ujenzi awamu ya nne hadi tarehe 12/05/2022
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa