Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na utoaji wa misaada kwa Jamii Good Neibhours Tanzania imeandaa Mafunzo maalumu kwa walimu wa masomo ya Sayansi,Hesabu na Kiingereza kwa shule za Sekondari Kimbiji na Pembamnanzi ,Mafunzo ni ya siku tatu kuanzia tarehe 11 June-13 June yanayofanyika katika fukwe ya bahari ukumbi wa Barakuda
Aidha lengo la kuandaa Mafunzo hayo ni kuwajengea walimu hao uwezo wa Umahiri katika Mtaala Mpya ulioboreshwa katika masomo na ufundishaji.
Mafunzo hayo ambayo yalifunguliwa na Bi,Twidike Ntwima Afisa Elimu kata ya Kimbiji Amesema
"Kipekee nawapongeza na kuwashukuru sana shirika la Good Neibhours Tanzania Kwa kuandaa Mafunzo haya ya kuwajengea uwezo walimu wa masomo ya Sayansi,Hesabu na Kiingereza na ameomba wawe na muendelezo wa kuandaa semina mara kwa mara kwani kupitia Mafunzo haya wanafunzi watanufaika kwa kuongeza ufaulu kwa kupitia Ujuzi ,maarifa na mbinu walizozipata walimu katika mafunzo.
Pia nimewataka walimu waliopata Mafunzo haya yakawe chachu kwa walimu wengine na pia kuwafundisha wanafunzi wa juhudi zote na kutumia mtaala wa Umahiri yaani (Competence -Based Curriculum),Alisema Bi Twidike Ntwima Afisa Elimu kata ya Kimbiji.
"Kipekee kama shirika Letu lilivyo Tunaendelea kutoa misaada mbalimbali katika Jamii yetu leo tumeandaa Mafunzo haya maalum kwa walimu wa 20 wa Sekondari Kimbiji na Pembamnanzi Lengo kuu ni kuwajengea uwezo kuweza kutumia mbinu mbalimbali
za mtaala wa Umahiri tunafahamu Mtaala imedhamiria wanafunzi wafundishwe mbinu shirikishi.
Pia kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia mihutasari kwani ndiyo msingi wa masomo katika ufundishaji,, Alisema Bi.Anameleni Christian mkufunzi mwandamizi wa shirika la Good Neibhours
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa