Habari picha ikiwaonesha baadhi ya wachinjaji na wachunaji wa ngozi za N'gombe na Mbuzi wakipatiwa mafunzo ya namna bora kuendesha shughuli zao ikiwa ni pamoja na uhifadhi, aina za ngozi pamoja na uchinjaji salama wa mifugo hiyo ili kulinda afya ya walaji.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Januari 28. 2026 katika ukumbi mdogo wa mikutano (Boardroom) uliopo ndani ya jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ikiwa ni maandalizi ya ufunguzi wa machinjio ya kisasa ya bamba iliyopo Kata ya Somangila, Wilayani humo.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya kilimo mifugo na uvuvi Bi. priscila Muhina amewataka wachinjaji na wachunaji hao kuhakikisha wanakata leseni za kuendesha shughuli zao ili waweze kutambulika, huku akiwaasa kuchangamkia fursa za kiuchumi zitakazopatikana kutokana na kufunguliwa kwa machinjio hiyo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa