Wananchi wa mtaa wa Tungwi-Songani Kata ya Pembamnazi Manispaa ya Kigamboni wametakiwa kutunza miundombinu ya soko ili soko liweze kudumu kwa muda mrefu na kunufaisha wananchi wote kwa ujumla.
Rai hiyo imetolewa ijumaa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Maabadi Hoja alipokuwa akizindua mradi wa soko hilo lililojengwa Mtaa wa Tundwi-Songani , alisema kuwa mradi huu umenza ujenzi muda mrefu tangu mwaka 2002, hivyo tunatarajia ukamilikaji wake utaleta maendeleo kwa wananchi wote wa Tundwi Songani na jamii nzima ya Kata ya PembaMnazi hivyo ni muhimu kuhakikisha unatunzwa.
Alisema kuwa ulinzi uimarishwe wa miundombinu na kuhakikisha lengo lililokusudiwa la kuboresha mazingira na utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara na wananchi wa Tundwi na kata ya Pemba Mnazi kwa ujumla linafikiwa.
Akitoa taarifa ya mradi Mratibu wa TASAF Manispaa ya kigamboni Bi.Janet Kacholi alisema kuwa, mradi wa soko ni miongoni mwa miradi iliyoibuliwa na wananchi kupitia program ya TASAF, ambapo umelenga kutoa ajira kwa vijana kwa kupata fursa ya kuuza mazao mbalimbali na kuiwezesha Serikali kupitia Halmashauri kukusanya mapato kutokana na ushuru mbalimbali utakaotozwa kwa wafanyabiashara.
Aliongeza kuwa hadi kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo jumla ya Tsh.91,858,842.24 zimetumika ambapo wananchi wamechanga kiasi cha Tsh.34.040.427.27 mchango wa TASAF ni Tsh.26,416,827.27 na Halmashauri ya Manispa ya kigamboni imetoa Tsh.31,401,587.7 ambazo zimekamilisha ujenzi wa meza za ndani baada ya Halmshauri ya Temeke kushindwa kutoa fedha za ukamilishaji kama ilivyoahidi wakati wa uibuaji wa mradi kabla ya kugawanywa.
Soko lipo tayari kwa matumizi ambapo vizimba /meza 60 sawa na wafanyabiashara 60 wataweza kufanya biashara ndani ya soko hilo na eneo la nje kuzunguka soko linakadiriwa kuchukua wafanyabisahara 80 ikiwa watapangwa na kusimamiwa vizuri.
Aidha Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Tundwi Bw. Mikdadi Simba alisema kuwa wananchi wamelipokea soko kwa mikono miwili na litawaletea maendelo kwa sababu wataweza kufanya biashara kisasa zaidi kwa kuzingatia mji unapanuka.
Mfanyabiashara Rehema Kambi amesema tunashukuru kwa mradi huu wa soko kwani tunauhakika wa usalama wa bidhaa zetu hazitaweza kuharibiwa kwa mvua kama kipindi cha nyuma hivyo tunaomba Manispaa ituletee miradi mingine mizuri zaidi ya huu.
Mwenyekiti wa mtaa wa Tundwi Bw.Rajabu Kihimbo aliongeza kuwa anaiomba manispaa ione namna ya kuwasaidia kwenye suala la umeme ili waweze kuimarisha ulinzi na wafanyabiashara waweze kufanya biashara hata nyakati za usiku.
Uzinduzi wa soko umekuja mara baada ya kukamilika kwa ujenzi uliohusisha awamu mbili awamu ya kwanza ikiwa ni ujenzi wa jengo la soko , vyoo na nyumba ya kuhifadhia vifaa mbalimbali na awamu ya pili ujenzi wa vizimba.
muonekano wa soko kwa nje.
Mratibu wa TASAF Manispaa ya Kigamboni Bi.Janet Kacholi akisoma taarifa ya mradi wa soko.
Baadhi ya wananchi waliofika kushiriki uzinduzi wa soko
Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Maabadi Hoja akizindua soko kwa kufungua kibao chenye maandishi ya uzinduzi wa soko hilo.
Meya wa Manispaa ya kigamboni Mh.Maabadi Hoja akisoma maandishi ya kibao cha uzinduzi mara baada ya kuzinduz kwa kutoa kitambaa.
Mathiki meya na wananchi wakisoma maandishi ya kibao cha uzinduzi wa soko hilo.
Mstahiki Meya Manispaa ya Kigamboni Mh. Maabadi Hoja akikata utepe ishara ya uzinduzi wa soko na wananchi wakishuhudia
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Maabadi Hoja akikagua soko kwa ndani pamoja na wananchi.
Mastahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh. Maabadi Hoja akizungumza na wananchi wa Tundwi Songani mara baada ya kuzindua soko.
Mwananchi wa Tundwi Bi.Rehema Kambi akishukuru uongozi wa manispaa kwa kufungua soko hilo litakalowasaidia kuhifadhi mazao yao katika hali ya usalama.
Meya wa Manispaa ya kigamboni akiwa ameambatana na wananchi wakitoka eneo la soko mara baada ya uzinduzi.
Mweyekiti wa mtaa wa Tundwi akitoa shukurani kwa kuzinduliwa soko ambalo litawasaidia wananchi
Meya wa Manispaa ya Kigamboni akisalimiana na mwananchi mara baada ya kumaliza uzinduzi.
Mzee Omary Shomvi mkazi wa mtaa wa Tundwi akisisitiza uongozi wa Manispaa kuwek umeme kwenye soko kwaajili ya kuimarisha usalama.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa