“Nauagiza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kuhakikisha utoaji wa huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni unaanza rasmi ifikapo siku ya jumatatu tarehe 1/06/2020.”
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa, Paul Makonda wakati akikabidhi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch. Ng’wilabuzu Ludigija msaada wa Magodoro 170, Mashuka 1,249 Mito 196, Vyandarua 201, Ndoo za kudekia 70, Madekio 48, Mafagio 96 pamoja na Vikamulio vya madekio 81 alivyovitoa ikiwa ni juhudi zake za kuisaidia Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni.
Aidha Mheshimiwa Makonda ameahidi kuleta mashine za Ultra sound mbili (2) zenye thamani ya Shilingi Milioni 70 na pia amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa Mkoa Dokta Rashid Mfaume kuleta watumishi wa Afya 40 ili kusogeza huduma kwa Wananchi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa