IJUE MIRADI YA ELIMU MSINGI ILIYOKAMILIKA KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022 KUTOKANA NA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imeendelea kutekeleza maagizo ya serikali ya kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 kupitia mapato yake ya ndani kukamilisha miradi kadhaa ya elimu msingi katika Manispaa hiyo na miradi mingine ikiendelea kutekelezwa.
Katika kata ya Pembamnazi Manispaa imejenga na kukamilisha ujenzi wa madarasa 2 shule ya msingi Buyuni ambapo hadi kufikia juni 2022 mradi huo ulikuwa umekamikika na kuanza kutumika kiasi cha shilingi mil.40 zimetumika ,pia mil.54,720,000 zimetumika kujenga madarasa 3 katika shule ya msingi Kichangani na madawati 60 yametengenezwa.
Aidha katika kata ya Kigamboni Manispaa imemalizia ujenzi wa madarasa 2 na ujenzi wa darasa 1 shule ya msingi Rahaleo pamoja na utengenezaji wa madawati 50 .Jumla ya shilingi mil.40 zimetumika.
Kata nyingine ni kata ya Kimbiji ambapo limejengwa darasa 1 na madawati 25 yametengenezwa na mradi umekamikika na kuanza kutumika Jumla ya shilingi mil.20 zimetumika.
Kwa upande wa kata ya Mjimwema shule ya msingi Kibugumo umaliziaji wa ujenzi wa madarasa 2 umefanyika na madawati 50 yametengenezwa na kuanza kutumika.Gharama iliyotumika ni mil.27,413,900.
Kata ya Vijibweni ujenzi wa umaliziaji madarasa 2 umefanyika katika shule ya msingi Kisiwani,Jumla ya mil.30,143,500 zimetumika na madawati 50 yametengenezwa.
Kata ya Kisarawe II Shule ya Msingi Chekeni Mwasonga Halmashauri imetoa kiasi cha shilingi mil.44,024,000 kwa ajili ya umaliziaji wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum ambapo fedha zingine zilitoka serikali kuu kiasi cha shilingi mil.80.
Utengenezaji wa Madawati 505 umefanyika katika kata ya Kibada ambapo shule zifuatazo zimenufaika na madawati hayo,shule hizo ni shule ya msingi Darajani,Ungindoni,Kibugumo,Mbutu, Vijibweni,Vumilia ukooni,Gomvu,Kimbiji,Kijaka,Kisarawe II,Mizimbini,Juhudi na Kibada.Jumla ya shilingi millioni 48 zimetumika.
Hongera Mkurugenzi na Menejimenti kwa kukamilisha miradi hii.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI KGMC.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa