Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe Ummy Mwalim, leo tarehe 27 July 2017 amezindua utoaji wa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee wa wilaya ya Kigamboni.na kuwapongeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni kwa kuweza kufanya utambuzi wa wazee zaidi ya elfu Saba ambapo nusu yao wamepatiwa vitambulisho vya matibabu bure.
Pamoja na uzinduzi wa zoezi hilo, Waziri Ummy amezitaka Halmashauri zote kuiga mfano wa Kigamboni na kuagiza kuwa kufikia tarehe 30/9/2017 wilaya zote nchini ziwe zimewatambua wazee katika maeneo yao na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bure.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa