MANISPAA YA KIGAMBONI YAFANYA KIKAO CHA KAWAIDA CHA BARAZA LA MADIWANI,LAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI ,WAPONGEZA KASI YA ULIPAJI FIDIA KWA WANANCHI
Leo 1/2/2022 Manispaa ya Kigamboni imefanya Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliofunguliwa na Mstahiki Meya wa Manispaa na kuhudhuriwa na Madiwani, Mkurugenzi na watendaji wa Manispaa ambapo moja ya ajenda ilikuwa ni kupokea taarifa za utekelezaji wa kazi katika kata kwa kipindi cha robo ya pili Oktoba hadi Disemba.
Katika mkutano huo kila Diwani amewasilisha taarifa za utekelezaji za Kata yake kisha kupitiwa na kujadiliwa na Baraza.
Wakijadili taarifa hizo za utekelezaji wa shughuli za Manispaa Madiwani wamepongeza Kasi ya ulipaji wa fidia kwa Kwa wananchi wa Gezaulole ambao serikali ulichukua eneo Lao Kwa ajili ya upimaji viwanja ,akiongelea suala Hilo Diwani Mh.Sanya amesema Kasi ya ulipaji ni nzuri hivyo amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa Erasto Kiwale kuendelea na Kasi hiyo hatimae kumaliza zoezi hilo.
Aidha wamepongeza jitihada za Mkurugenzi katika utoaji wa mikopo Kwa vikundi vya vijana,wanawake na walemavu,akinukuu amesema wamefurhishwa na kupewa mkopo kikundi cha Two in one kilichopo Kata ya Somangila kinachojishughulisha na shughuli za usafi ambacho kimepewa mkopo wa Tshs.Mil.55 Kwa ajili ya kununua gari la kukusanya taka.
Akifunga Mkutano huo Mstahiki Meya Mh.Ernest Ndambo Mafimbo amewataka watendaji kusimamia na kutekeleza maagizo na kupitia ushauri ambao umetolewa na Baraza.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa