Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli leo tarehe 13/09/2017 amefuta rasmi iliyokuwa Mamlaka ya uendelezaji wa mji mpya wa Kigamboni (Kigamboni Development Agency-KDA) na kukabidhi majukumu yote kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Pamoja na hayo Mh.Lukuvi ametangaza kuwa Mh.Rais Dr.John Pombe Magufuli amefuta umiliki wa shamba la Hekari 700 iliyokuwa inamilikiwa na mfanyabiashara Yusuf Manji iliyopo kata ya Somangila Manispaa ya Kigamboni pamoja na Shamba la Hekari 13000 iliopo kata ya Pembanmnazi.
Mh.Lukuvi amesema kuanzaia sasa Mashamba hayo yapo chini ya umuliki wa Serikali na hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kufanya shughuli yoyote katika mashamba hayo.
Kwa upande wake Mbunge wa Kigamboni Mh.Dr.Faustine Ndungulile amemshukuru Mh. Waziri kwa hatua hiyo kwani kumekuwa na kilio cha muda mrefu cha wananchi ambao maeneo yao yaliainishwa katika mpango huo ambapo kutokana na Maelekezo ya Serikali kuanzia mwaka 2008 hakuna Mwananchi yeyote aliyeruhusiwa kujenga wala kuendeleza eneo lake wakisubiri maelekezo ya serikali.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa