Katibu Wa Afya kutoka TAMISEMIDk.Dorothy Gwajima amepongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa utendajiKazi na hatua waliyopiga kwenye Ujenzi Wa hospital ya Wilaya na namna utoaji Wahuduma na uboreshwaji Wa mazingira ya Hospitali ya Vijibweni ulivyofanyika.
Katibu Wa Afya amesema hayo leoalipotembelea Ujenzi Wa hospitali ya Wilaya nautoaji Wa huduma Vijibweni na kueleza kuwa ameridhishwa na hali ya Ujenzi nakwamba hatarajii wakati Wa kukabidhi majengo hayo kuwepo na visingizio Vyakutokukamilika kwa mradi.
Aidha amepongeza hali ya usafi Wahospitali ya VIJIBWENI kuanzia mazingira , hali ya vitanda na magodoro.
Katibu Wa Afya pia ametoa siku 14kwa hospitali zote nchini kuhakikisha zinafanya maboresho ya vitanda, magodorona makava yake ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaolazwa .
Mara baada ya kutembelea maabara yavijibweni katibu Wa afya ametoa siku 7 kuhakikisha mashine ya kupimia homoniinapatikana na siku 30 kuhakikisha ufumbuzi Wa chumba kitakachokuwa kinatumikakupima ugonjwa Wa taifodi unapatikana ili wananchi wanaohitaji huduma hizowasipate usumbufu.
Dk.Dorothy amewapongeza timu yausimamizi Wa afya CHMT ya Kigamboni kwa kufanya maamuzi ya kukopa Fedha nakununua mashine ya Xray ambayo itatumika kwenye hospitali ya Vijibweni nakusema kuwa wamethubutu na wanaonesha wanaunga mkono juhudi za Serikali zauboreshaji Wa huduma za Afya.
Aidha amewataka watumishi Wa afyawaliofanya onesho la ukoaji Wa mama mjamzito aliyekumbwa na ugonjwa Wa kifafacha mimba wakati Wa kujifungua kuandaa makala ya video ili iweze kusambazwakwenye maeneo mengine waweze kujifunza namna ya kuokoa maisha ya mama na mtotoikitokea hali hiyo.
Mwisho Amewataka timu ya usimamiziWa afya ya Wilaya na mkoa kufanya Kazi kwa kushirikiana na kuwa wabunifu katikakutatua changamoto zinazokuwa zinawakabili kwenye maeneo yao ya Kazi.
Dkt. Dorothy Gwajima wa kwanza mbele akiwa amaembatana na Mganaga Mkuu wa Wilaya na wataalamu wengine wakitoka kutazama maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya .
Dkt. Dorothy Gwajima Katikati akiwa ameambata na madakatri na mganag amkuuwa Wilaya (kulia) wakitembelea maeneo ya utoaji wa huduma Hopsitali ya Vijibweni.
Dkt. Dorothy Gwajima akipata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa maabara
Dkt. Dorothy Gwajima akitoa maelekezo kwa mfamasia wa Hospitali ya Vijibweni kuhusiana na uagizaji wa dawa ili ziwepo wakati wote.
Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Vijibweni mara baada ya kumaliza ziara yake.
Katibu wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima akitoa maelekezo kwa watumishi wa hospitali Vijibweni
Picha ya pamoja na watumishi wa Hospitali ya Vijibweni.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa