• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Care Values
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu ya awali na Msingi
      • Kilima mifugo na umwagiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Sekondary
      • Mipango na uratibu
      • Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda biashara na Uwekezaji
      • Miundombinu ,Vijijini na Mjini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa jamii na Lishe
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
        • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa ndani
      • Usimamazi wa Manunuzi
      • Maliasili na uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na uhasibu
      • Usimamizi na usafi wa Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Utumishi
    • Huhuma za Kisheria
    • Usafi wa mazingira na udhibiti wa taka ngumu
    • Michezo na Sanaa
  • Madiwani
    • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
      • Huduma za jamii
    • Ratiba za Vikao
      • Vikao vya Waheshimiwa
      • Kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
      • Miradi ya Sasa
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Picha
    • Hotuba
    • Gazeti la Mtandaoni
    • Vipeperushi
  • Mifumo

KAMATI YA USHAURI WILAYA YA KIGAMBONI YAIDHINISHA BAJETI

Posted on: February 17th, 2023

KAMATI YA USHAURI WILAYA YA KIGAMBONI YAPITIA RASIMU YA BAJETI 2023/2024 NA KUIDHINISHA TSHS BIL.57.4


Leo tarehe 16/2/2023 Kamati ya ushauri ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Halima Bulembo imekaa kikao chenye lengo la Kupitia Rasimu ya Bajeti ya 2023/2024 .


Akiongea katika kikao hicho mara baada ya kujitambulisha amewapongeza wote kwa namna moja ama nyingine waliofanikisha kutekeleza kwa miradi ya maendeleo akiwepo Mkurugenzi na watumishi wote wa Manispaa katika utekelezaji wa miradi .


Akizungumzia lengo la kikao amesema lengo ni kupokea na kujadili mapendekezo ya Rasimu ya Bajeti ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Manispaa amesema anategemea maoni yao katika kupitia Rasimu hii ambayo yatakuwa yenye kujenga Kwa ajili ya maendeleo ya Manispaa.


Aidha amemtaka meneja wa TARURA kufanya ushawishi ili kuongeza Bajeti ya barabara angalau kufikia lengo,pamoja na Hilo amewataka wananchi kuacha kukopa mikopo ya Kaushal damu kwani si sahihi hivyo amewataka viongozi ngazi zote kuwaelimisha wananchi kutojiiingiza katika mikopo hiyo kwani inawaingiza katika matatizo na haiwasaidii kujikwambua kwa kuanzisha biashara hivyo amewataka kujikita katika mikopo ya Halmashauri ambayo haina riba kabisa.


Akiwapitisha wajumbe katika Rasimu hiyo Mchumi wa Manispaa ya Kigamboni  bi.Flora Nyanana amesema Bajeti hiyo imezingatia muongozo elekezi na ikilinganishwa na ya mwaka Jana imeongezeka kwa asilimia 25.Akitaja moja ya mikakati wa kuongeza mapato amesema itajengwa hostel ya kisasa ya ghorofa kwa ajili ya kuwapunguzia adha wanafunzi.


Akiongea Mbunge wa Kigamboni amesema kwa upande wa suala la Michezo kuna Juhudi nyingi zimefanyika kuhamasisha Wadau kuja kuendeleza Michezo moja wapo ni Machava ambapo kuna kiwanja kizuri cha mpira wa kikapu kwa msaada wa Wadau .Kwa upande wa barabara amesema barabara itajengwa kiwango cha lami  kupitia mradi wa DMDP  kilomita 100 za barabara  katika  Kata zitajengwa katika kiwango cha lami  kufikia mwishoni mwa mwaka utekelezaji huo utakuwa unaanza,lakini pia katika kutatua tatizo la kuchonga barabara Manispaa imejipanga katika Bajeti hii itanunua greda ambalo litatatua kero ya uchongaji wa barabara.Aidha Bajeti hii itaenda kuongeza na kuboresha huduma za mama na mtoto.


Akiongea Meya wa Manispaa Mh.Ernest Mafimbo amegusia suala la mikopo kuchukua muda tofauti na mikopo ya mitaani amefafanua kuwa mikopo hii hutolewa kwa kila Robo hivyo ndani ya mwaka hutolewa mara nne na hufuata utaratibu maalum hadi kumfikia mkopaji.



Wakitoa maoni mbalimbali wajumbe hao wameongeza utekelezaji wa miradi ya Elimu na afya katika Manispaa ya Kigamboni,lakini pia wametaka Bajeti  kujikita pia katika maswala ya Michezo kwani Michezo ni ajira ,miundo mbinu ikiwepo barabara kuhakikisha zinajengwa kwa kiwango cha lami hivyo pesa ziwekwe kwa kuzingatia hilo ikiwepo mitaro ili kudhibiti suala la mafuriko aidha katika Bajeti upande wa maendeleo ya jamii wametaka Bajeti ijikite katika kutekeleza shughuli za kudhibiti maadilibkwani maadili katika jamii yameshuka .


Nae Mkurugenzi ndg.Erasto Kiwale akifafanua baadhi ya maoni yaliyotolewa na wajumbe katika suala la Michezo na Machinjio amesema kuna yaliyofanyiwa kazi tayari mfano suala la machinjio ilishaanza kujengwa katika Kata ya Somangila na ujenzi upo katika hatua ya upauaji na ujenzi unaendelea,na kuhusu Michezo amesema Juhudi zimefanyika katika ufukwe wa umma wa Kidete imetengwa sehemu ya uwanja na kuwekwa magoli na tayari unatumika kwa mpira wa miguu.


Akifunga kikao hicho DC Bulembo amewashukuru wajumbe na kuwaomba ushirikiano wa dhati  ili kuendeleza Kigamboni na kufikia malengo kwa urahisi.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini KGMC

Matangazo

  • Tangazo la Frem za Biashara, Soko la Kibada February 26, 2025
  • Tangazo la kuitwa kwenye usaili nafasi ya mwendesha mashine ya Bayometriki na Mwandishi msaidizi February 24, 2025
  • Tangazo la uteuzi wa wajumbe wa bodi ya Afya March 26, 2025
  • Tangazo la kuitwa kazini nafasi ya mwendesha mashine ya Bayometriki na Mwandishi msaidizi March 12, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE. DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIBADA - MWASONGA

    April 25, 2025
  • MANISPAA YA KIGAMBONI IMEPOKEA VITI MWENDO 35 NYENYE THAMANI YA TSH MIL 8

    April 08, 2025
  • MKANDARASI TOKA SUMA JKT ATAKIWA KUANZA MAPEMA MAANDALIZI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA TUNGI

    April 08, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele amefanya ziara ndani ya Manispaa ya Kigamboni

    March 22, 2025
  • Angalia Zote

Video

Makala maalumu ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Kigamboni
Video zingine

Kurasa za karibu

  • Municipal councilors
  • Kigamboni Municipal History
  • Investment Opportunities
  • Fomu ya Maombi ya Kiwanja
  • Huduma za Afya na Orodha ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni

    Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam

    Simu: +255222928468

    Simu ya Mkononi: +255222928468

    Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa