NEEMA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM KIGAMBONI,DC FATMA A.NYANGASA AZUNGUMZA
Hilo limejulikana leo hii 21/9/2022 wakati Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Fatma Almas Nyangasa akizungumza alipotembelea na kufanya ukaguzi Mradi ujenzi wa bweni la wasichana wenye mahitaji maalum lililopo Chekeni Mwasonga shule ya Msingi.
Akizungumza katika ziara hiyo amesema ni matarajio kuwa kuanzia January mwakani shule
hiyo ambayo inakuwa shule ya yabkwanza ya watoto wenye mahitaji maalum itaanza ambapo kwa Kigamboni hakukuwa na shule ya wenye mahitaji hivyo ni Mradi mkubwa na wa kujivunia
,sambamba na hilo yataongezwa
madarasa mengine mawili na mengine manne yatafanyiwa ukarabati tayari kwa ajili ya kuanza kutumika hiyo January Mradi huo umekamilika
kwa 95% na utagharimu shilingi
mil.127 ambazo mil.80 ni pesa za
uvico 19 na mil.47 na 24 elfu
ni fedha za mapato ya ndani ya Manispaa ya Kigamboni.
Aidha amesema kwa bajeti hii ya 2022/2023 kiasi cha bil.1.937 zimetengwa kwa ajili ya miradi elimu mipya na ukarabati wa miradi ya shule za Msingi kwa Wilaya ya Kigamboni,kutokana na hilo amemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezeaha Kigamboni kupata fedha hizo kwa ajili ya Miradi ya elimu.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI KGMC
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa