• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Care Values
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu ya awali na Msingi
      • Kilima mifugo na umwagiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Sekondary
      • Mipango na uratibu
      • Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda biashara na Uwekezaji
      • Miundombinu ,Vijijini na Mjini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa jamii na Lishe
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
        • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa ndani
      • Usimamazi wa Manunuzi
      • Maliasili na uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na uhasibu
      • Usimamizi na usafi wa Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Utumishi
    • Huhuma za Kisheria
    • Usafi wa mazingira na udhibiti wa taka ngumu
    • Michezo na Sanaa
  • Madiwani
    • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
      • Huduma za jamii
    • Ratiba za Vikao
      • Vikao vya Waheshimiwa
      • Kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
      • Miradi ya Sasa
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Picha
    • Hotuba
    • Gazeti la Mtandaoni
    • Vipeperushi
  • Mifumo

DC Kigamboni aondoa hali ya taharuki kwa wakazi wa kibada juu ya bomoabomoa

Posted on: May 3rd, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa ameondoa hali ya taharuki iliyokuwa imetanda miongoni mwa wananchi wa Kata ya Kibada waliowekewa alama ya kubomoa majengo yao na  wakala wa barabara (TANROADS) mbali na kununua viwanja hivyo kihalali kutoka wizara ya ardhi.

Akizungumza na wananchi hao kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye ofisi za Kata ya Kibada Mh.Mgandilwa amesema kuwa ofisi yake na wataalamu hawapo tayari kuona wananchi wao wanaonewa.

Aliongeza kuwa mgongano huo umebainika kwenye mradi wa ujenzi wa barabara uliopo kwenye hatua za awali na ubainishaji wa mipaka wa Tanroads unaolenga kujenga barabara kiwango cha lami kuanzia Kibada-Somangila hadi Kimbiji.

Mgandilwa alisema kuwa wizara ya ardhi ilikuwa na mradi wa viwanja ishirini elfu vilivyouzwa kwa wananchi kihalali ambapo baada ya Tanroads kubainisha mipaka yake ndipo ilipobainika kuwa wizara ya ardhi iliuza viwanja vyake hadi kwenye hifadhi ya barabara.

"Viwanja hivi vilinunuliwa wizara ya ardhi ambapo wananchi walikuwa na uhakika wa usalama wa viwanja vyao kutokana na kununua kwene wizara husika, leo hii kuja kuwawekea alama ya kubomoa sio haki, mwananchi anakuwa anawajibishwa kwa kosa ambalo si lake ndiomaana tumekutana hapa ili tuweze kuona namna gani tunaweza kufikia muafaka" Alisema Mkuu wa Wilaya.

Aliongeza kuwa wao kama Serikali wameona ni bora kuzungumza na wananchi  kwasababu Serikali haipaswi kukinzana na sheria badala yake inaangalia mahali ambapo pamekosewa na kurekebisha.

Aidha Mkuu wa Wilaya aliwataka wananchi wote waliowekea alama za kubomoa majengo yao ndani ya siku 90 kufika ofisini kwake siku ya jumamosi tarehe 5/5/2018 ambapo kutakuwa na wataalamu kutoka wizara ya Ardhi na Tanroads ili kuona namna bora ya kufikia muafaka.

Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye hamasa na kuthaminiwa hususani wananchi ambao watapitiwa na ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoozea umeme ambapo italazimika kusimika nguzo za umeme ambazo hazitaruhusu uwepo wa makazi ya aina yeyote.

Mkuu wa Wilaya alisema kuwa, ni vyema wakajitokeza ili kuondoa malalamiko na adha zinazazoweza kuzuilika kwenye hatua za utambuzi na uthamini ili kulipwa fidia kwasababu nishati ya umeme inahitajika kwa kiwango kikubwa kutokana na Wilaya ya Kigamboni kukosa umeme wa uhakika, na kuwa waathirika wa kwanza pindi inapotokea hitilafu kidogo kwenye vituo vinavyotegemewa kwa sasa.

"Nawaomba ndugu zangu mjitokeze pindi mtakapohitajika kwenye zoezi la utambuzi na uthamini, Wilaya ya kigamboni tunahitaji umeme wa uhakika ili tuweze kuwa na viwanda na uwekezaji wenye tija kutokana na kuwepo kwa umeme wa uhakika" Alisema Mh.Mgandilwa

Mradi wa kituo kidogo cha kuupozea umeme kinajengwa Dege kata ya Somangila ambapo hadi kufikia mwaka 2020 unatarajiwa kuwa umeanza kazi huku Kata tatu za Kibada,KisaraweII na Somangila kwenye mitaa 6 inatarajiwa kupitiwa na nguzo hizo zenye umeme mkubwa ambao hauruhusu kuwepo kwa makazi yeyote kwa usalama wa wananchi wa maeneo hayo.

Uchimbaji wa kutafuta mawe ya mipaka kwenye eneo la mwananchi wa Kibada, Mh.Amin Sambo Diwani wa Kata ya Kibada akishiriki kwa kuchimba

Mkuu wa Wilaya Mh.Hashim Mgandilwa akielekeza jambo mara baada ya kufika kwenye moja ya jiwe la mpaka lililokuwa likitafutwa

Mkuu wa Wilaya Mh.Hashim Mgandilwa aliyevaa kofia nyeusi pamoja na wakazi wa Kibada wakisoma ramani kubaini mipaka

Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Wilaya na wananchi wakizuru kuangalia mawe ya mipaka yaliyopo kwenye eneo hilo ambapo nyumba imewekewa alama ya kubomoa.

Utafiti wa mawe ya mipaka ukiendelea kwenye moja ya nyumba iliyowekewa alama ya kubomoa Kata ya Kibada.

wataalamu na wananchi wakisilikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya alipokuwa akizungumza

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa akizungumza na wananchi wa Kata ya kibada na kutolea ufafanuzi wa alama za ubomoaji zilizowekwa kwenye majengo yao na wakala wa barabara Tanroads

Mwananchi Bw.Asaa Simba mkazi wa Kibada akitoa maoni yake kwa Mkuu wa Wilaya aliyefika kuzungumza juuya bomoa bomoa

Mthamini wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Mpoki Daimon akitoa malekezo ya ulipwaji wa fidia na vigezo vyake kwa wananchi wa Dege Kata ya Somangila

muonekano wa kituo kidogo cha kufulia umeme Dege kikiwa kwenye hatua za awali za ujenzi

Matangazo

  • Tangazo la Frem za Biashara, Soko la Kibada February 26, 2025
  • Tangazo la kuitwa kwenye usaili nafasi ya mwendesha mashine ya Bayometriki na Mwandishi msaidizi February 24, 2025
  • Tangazo la uteuzi wa wajumbe wa bodi ya Afya March 26, 2025
  • Tangazo la kuitwa kazini nafasi ya mwendesha mashine ya Bayometriki na Mwandishi msaidizi March 12, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE. DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIBADA - MWASONGA

    April 25, 2025
  • MANISPAA YA KIGAMBONI IMEPOKEA VITI MWENDO 35 NYENYE THAMANI YA TSH MIL 8

    April 08, 2025
  • MKANDARASI TOKA SUMA JKT ATAKIWA KUANZA MAPEMA MAANDALIZI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA TUNGI

    April 08, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele amefanya ziara ndani ya Manispaa ya Kigamboni

    March 22, 2025
  • Angalia Zote

Video

Makala maalumu ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Kigamboni
Video zingine

Kurasa za karibu

  • Municipal councilors
  • Kigamboni Municipal History
  • Investment Opportunities
  • Fomu ya Maombi ya Kiwanja
  • Huduma za Afya na Orodha ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni

    Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam

    Simu: +255222928468

    Simu ya Mkononi: +255222928468

    Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa