• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Care Values
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu ya awali na Msingi
      • Kilima mifugo na umwagiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Sekondary
      • Mipango na uratibu
      • Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda biashara na Uwekezaji
      • Miundombinu ,Vijijini na Mjini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa jamii na Lishe
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
        • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa ndani
      • Usimamazi wa Manunuzi
      • Maliasili na uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na uhasibu
      • Usimamizi na usafi wa Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Utumishi
    • Huhuma za Kisheria
    • Usafi wa mazingira na udhibiti wa taka ngumu
    • Michezo na Sanaa
  • Madiwani
    • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
      • Huduma za jamii
    • Ratiba za Vikao
      • Vikao vya Waheshimiwa
      • Kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
      • Miradi ya Sasa
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Picha
    • Hotuba
    • Gazeti la Mtandaoni
    • Vipeperushi
  • Mifumo

DC BULEMBO AWEKA WAZI HATUA ZILIZOFIKIWA UTATUZI MGOGORO WA BARABARA YA KIDAGAA MTAA WA MIKENGE - KIMBIJI, AELEZA UMUHIMU VIBALI VYA UJENZI

Posted on: July 4th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo ameendelea na ziara yake ya kutambua kero za  mtaa kwa mtaa ambapo leo tarehe 14 Juni, 2023 amefika katika mitaa ya Mikenge,Kizito huonjwa na Ngobanya ndani ya Kata ya Kimbiji.

Katika kutatua changamoto za Wananchi, DC Bulembo ameweka wazi hatua zilizofikiwa ili kumaliza mgogoro wa barabara ya Kidagaa ulikuwa kati ya Wananchi na Mwekezaji Kampuni ya (ASM Limited) mgogoro ambao umedumu kwa muda mrefu.

 Tumefikia jitijhada kubwa sana haikuwa rahisi, niwaombe wana Mikenge mridhie tumepata barabara tatu tofauti zitakazokuwa zinaenda mpaka ufukweni na kwenye makazi ambapo mwanzo  barabara ilikuwa moja, niwasihi tusiwe na migogoro baina yetu kama Serikali, Wananchi na Wawekezaji, tuliongea na Mwekezaji (ASM) na yeye amekubali kuwajibika katika kutengeneza barabara itakayopita hadi baharini na tulimpa muda wa siku 90 atakamilisha* " Alisema DC Bulembo

Aidha DC Bulembo amemtaka Afisa Ardhi Manispaa ya Kigamboni kuwaandikia barua wawekezaji wote za kuwataka kuzingatia sheria na taratibu kwa kushirikisha serikali kupitia idara ya ardhi kwenye masuala ya tathmini kwa maeneo wanayonunua kwa wananchi ili kuepukana na migogoro mbalimbali kama dhulma.

Akijibu kero ya vyoo shule ya Msingi Mikenge DC Bulembo ameahiza Manispaa kumleta  Mhandisi wao kufika katika shule ya Mikenge kuona adha inayolalamikiwa ya ubovu wa vyoo ilikusudi kujua namna gani ya kuweza kurekebisha vyoo hivyo.

Nae Afisa elimu Msingi ndg.Hasaan Mianza ameweka wazi kwa wananchi( walipotaka kujua kuhusu kuongezwa kwa madarasa na uhaba wa walimu) kuwa zipo fedha kutoka kwenye Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 zimetengwa kiasi cha Tsh Milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa mawili katika shule ya msingi Mikenge, Aidha katika ajira mpya zilizotangazwa, Manispaa imeweka kipaumbele cha kuongezwa kwa walimu wawili katika shule hiyo.

Akijibu maswali ya Wananchi, Meneja DAWASA amesema katika bajeti ya 2023/24 zimetengwa fedha na kuanzia mwezi wa 9 ujenzi wa kupitisha mabomba ya maji safi kwa kilomita 5 utaanza  na kwa Kata ya Kimbiji utapitia katika mtaa wa Mikenge, Kizitohuonjwa na Kijaka.

Aidha, katika kutatua kero ya barabara zilizoharibiwa na mvua Manispaa ya Kigamboni imetolewa pesa kwa kila kata  kwa ajili ya  marekebisho ya kuchonga na kuweka vifusi katika barabara na tayari pesa hizo zimeshatolewa kwa ajili ya utekelezaji,kila Kata imepata kiasi cha shilingi mil 28 ambapo mil.18 kutoka TARURA ambazo tayari zimekwishapokelewa na mil.10 zitatoka Manispaa.                             Akijibu kuhusu ombi la kuondolewa kwa ukataji wa vibali vya ujenzi kunakoonekana kuwa ni kero    kwa wananchi Mh.Bulembo amesema vibali vya ujenzi vina umuhimu mkubwa Sana Katika kudhibiti migogoro ya ardhi, kudhibiti ujenzi holela  na upangaji wa mji  hivyo amewataka kuendelea kukata vibali vya ujenzi wanapotaka kuanzisha ujenzi wowote ili kuepuka usumbufu .                      

Katika kushiriki kwa vitendo kutatua kero za wananchi Mh.Bulembo amefanya Harambee kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mtaa ambapo katika mkutano huo zimepatikana pesa kiasi cha shilingi mil.ambapo Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile ,Mh.Bulembo,Mh.Sanya Bunaya Diwani wa Kimbiji na Mkurugenzi wa Manispaa ndg.Erasto Kiwale wamechangia  na wataalam pia alioambatana nao wameshiriki katika Harambee hiyo. 

Matangazo

  • Tangazo la Frem za Biashara, Soko la Kibada February 26, 2025
  • Tangazo la kuitwa kwenye usaili nafasi ya mwendesha mashine ya Bayometriki na Mwandishi msaidizi February 24, 2025
  • Tangazo la uteuzi wa wajumbe wa bodi ya Afya March 26, 2025
  • Tangazo la kuitwa kazini nafasi ya mwendesha mashine ya Bayometriki na Mwandishi msaidizi March 12, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE. DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIBADA - MWASONGA

    April 25, 2025
  • MANISPAA YA KIGAMBONI IMEPOKEA VITI MWENDO 35 NYENYE THAMANI YA TSH MIL 8

    April 08, 2025
  • MKANDARASI TOKA SUMA JKT ATAKIWA KUANZA MAPEMA MAANDALIZI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA TUNGI

    April 08, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele amefanya ziara ndani ya Manispaa ya Kigamboni

    March 22, 2025
  • Angalia Zote

Video

Makala maalumu ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Kigamboni
Video zingine

Kurasa za karibu

  • Municipal councilors
  • Kigamboni Municipal History
  • Investment Opportunities
  • Fomu ya Maombi ya Kiwanja
  • Huduma za Afya na Orodha ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni

    Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam

    Simu: +255222928468

    Simu ya Mkononi: +255222928468

    Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa