Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imepokea fedha kiasi cha bilioni 1.5 kutoka Serikali Kuu kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya itakayohudumia wananchi wote wa Kigamboni ambapo hapo awali Hospitali ya Wilaya haikuwepo.
Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya umeanza mwezi wa pili enepo la Gezauloole Kata ya Somangila na majengo yanayojengwa ni pamoja na jengo la Utawala, wazazi,OPD (wagonjwa wa nje),jengo la mionzi, maabara, stoo ya dawa na chumba cha kufulia nguo.
Kukamilika kwa ujenzi huu wa Hospitali ya Wilaya kutasaidia kuimarisha huduma za afya ngazi ya Wilaya,Ajira kwa wananchi wenye taaluma ya afya, mradi umesaidia kuajiri wafanyakazi waliohusika na ujenzi wa Hospitali, ukuzaji wa uchumi kwa wananchi wanaozunguka eneo la Hospitali kwa kupata fursa za kutoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa na wanaohudumia wagonjwa.
Hadi sasa Mradi upo kwenye hatua za Ukamilishaji .
|
||
Majengo ya Maabara na OPD kwa muonekano wa picha ya pamoja. |
|
Jengo la Utawala. |
|
||
Jengo la kuhifadhia dawa |
|
Jengo la kufulia nguo yaani (laundry room) |
|
||
Majengo ya maabara | ||
|
||
Majengo ya mama na mtoto | ||
|
||
Majengo ya wagonjwa wa nje yaani OPD | ||
|
||
Majengo ya mionzi. |
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa