• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Livestock na Fisheries
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Sekondary
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Mipango Mija na Maendeleo ya Ardhi
      • Afya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba za Vikao
      • Vikao vya Waheshimiwa
      • Kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ya Sasa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Picha za Video
    • Hotuba Mbalimbali
    • Picha

DC Sara awashukuru Kampuni ya KC kwa msaada wa mifuko ya simenti100

Posted on: January 7th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri leo ameishukuru kampuni ya KC LAND DEVELOPMENT PLAN CONSULATANT COMPANY LTD kwa msaada wa mifuko ya simenti 100 yenye thamani ya shilingi 1,500,000/= kwa lengo la kuunga mkono jitihada za kuboresha miundombinu ya elimu kwa wananchi wa Kigamboni.

Mkuu wa Wilaya amesema kuwa  anawashukuru wadau wa maenedeleo kwa kuweza kuja kuungana na wananchi na viongozi wa kigamboni kwa kuhakikisha guruduma la kutoa elimu bora linafanikiwa na kuongeza kuwa Mpaka sasa changamoto ya vyumba vya madarasa limekwisha changamoto iliyopo ni madawati ambayo nayo hivi karibuni yanatarajiwa kukamilishwa.

Mhe. Sara amesema KC wamekuwa wadau wa kwanza kufunguluia ujenzi wa Shule ya kisasa ya Msingi inayolengwa kujengwa kwenye eneo la makao makuu ya Wilaya Gezaulole ambapo Mkurugenzi amekwisha weka kwenye mpango wa bajeti ijayo.

 “Mifuko hii itakwenda kufyatuliwa kwenye kiwanda chetu cha matofali ambapo tunatarajia kupata madarasa matatu, Unapomsaidia mtoto elimu unakuwa umemsaidia yeye pamoja na familia yake, sisi tunawashukuru sana”.Alisema Mkuu wa Wilaya

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw. Msoses Chilla  amesema Mradi huo wa ujenzi wa Shule ya kisasa ya Msingi Gezaulole unatarajiwa hadi kufikia mwezi wa 12 uwe umekamilika ili kuruhusu watoto kuweza kusoma.

Ameongeza kuwa Msaada huo wa mifuko ya simenti umeifungulia njia Kigamboni hasa  Taasisi kama KC zinaposhirikiana na Serikali  inatoa faraja, hivyo anaendelea kuwakaribisha wadau wengine waweze kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha miundombinu ya Elimu na sekta nyingine zote.

Msemaji wa Kampuni ya KC Mussa Hussein amesema kuwa wameamua kuunga mkono jitihada za Serikali za kuongeza vyumba vya madarasa ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora na wao kama wadau wameguswa kutoa kidogo walinacho kwani wanatambua kuwa Elimu ni msingi na wanaahidi kuendelea kutoa ushirikiano.


Kaimu Mkurugenzi Bw. Mosses Chilla akishukuru Kc kwa msaada wa Matofali kwa msemaji wa kampuni ya KC

Msemaji wa KC Bw. Mussa Hussein akizungumzia lengo la kutoa msaada huo

Mifuko ya simenti ikishushwa na kuingizwa kiwandani.

Mtambo wa kufyatulia matofali.

muonekano wa kiwanda cha kufyatulia matofali.

Matangazo

  • TANGAZO LA UCHAGUZI WA WAJUMBE WA BODI YA AFYA YA HALMASHAURI NA KAMATI ZA AFYA ZA VITUO MANISPAA YA KIGAMBONI. December 03, 2020
  • MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE ZA SEKONDARI MANISPAA YA KIGAMBONI December 16, 2020
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • LEAT kushirikiana na Serikali kutatua changamoto za kimazingiraa kwa ustawi wa afya za wananchi

    January 20, 2021
  • Wajumbe wa Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango wapongeza Menejiment kwa usimamizi mzuri wa miradi.

    January 19, 2021
  • "Pikipiki hizi zitumike kuboresha utendaji kazi wa Serikali na si vinginevyo" Katibu Tawala Kigamboni,

    January 14, 2021
  • DC Sara awashukuru Kampuni ya KC kwa msaada wa mifuko ya simenti100

    January 07, 2021
  • Angalia Zote

Video

Makala ya Miradi ya Maendeleo Kigamboni Manispaa
Video zingine

Kurasa za karibu

  • Municipal councilors
  • Kigamboni Municipal History
  • Investment Opportunities
  • Fomu ya Maombi ya Kiwanja
  • Huduma za Afya na Orodha ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni

    Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam

    Simu: +255222928468

    Simu ya Mkononi: +255222928468

    Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa