1.0. UTANGULIZI
Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika ni kati ya Idara 13 za Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni. Idara hii ina sehemu kuu moja (1) ambayo ni sehemu ya Ushirika. Katika kuinua maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia katika kuongeza vyanzo vya ajira isiyo rasmi kwa wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni idara hii inachangia kwa:
• Kuhudumia na kutoa ushauri kwa wakulima kuhusu kilimo bora cha mazao mbalimbali.
• Kutoa elimu ya kilimo kwa njia ya umwagiliaji mdogo (watering) na mkubwa (scheme)
• Kutoa elimu juu ya lishe bora na usindikaji wa mazao ya kilimo
• Kuelimisha juu ya zana za kilimo na matumizi sahihi ya zana hizo
• Kutoa elimu ya ushirika na uhamasishaji wa kuundwa kwa vyama vya ushirika
• Kudhibiti na kuzuia wadudu na magonjwa ya mazao na mimea kwa njia ya Zahanati za Afya ya Mimea.
Hali ya Idara
Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika ina Wataalam kumi na saba (17) ambao ni wa kada na wenye fani mbalimbali:
Maafisa Kilimo 2
Maafisa Kilimo Wakuu Wasaidizi 7
Afisa Kilimo Mwandamizi Msaidizi 1
Maafisa Kilimo Wasaidizi 6
Afisa Ushirika Mkuu 1
Uwiano wa utoaji huduma kwa wataalam kwa wakulima katika Manispaa hii ni wakulima 1:760.
Idadi ya kaya za wakulima waliopo ni 3941 zenye jumla ya wakulima 12120 ambayo ni asilimia 7% ya wakazi wote 162932
Uchangiaji wa shughuli za kilimo kwa upatikanaji wa mazao mbalimbali ya kilimo ni kwa kiasi cha asilimia 30% ya mahitaji ya chakula kinachohitajika katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Wigo Wa Huduma zitolewazo
Eneo linalofaa kwa kilimo ni hektari 2100. Uzalishaji katika eneo hilo ni Mboga mboga za aina mbalimbali hektari 11,500.0, Minazi hektari 460.0, Michikichi 480.0, Mpunga 3040.0, Mahindi 500.0. Pia mazao aina ya mikorosho, migomba, miembe na kilimo mjini ambacho hujulikana pia kama kilimo cha maghorofani kwa kutumia vifaa mbalimbali kuotoshea na kuzalishia mimea mbalimbali na mazao yake kinafanyika hasa kwa familia ambazo hazina maeneo ya kulima bustani. Kilimo hiki kinatiliwa mkazo kwa kuwa kadiri muda unavyoenda maeneo ya kilimo yanaendelea kupungua na kugeuka kuwa makazi.
2.0 HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA IDARA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA
Utoaji wa elimu, ushauri na huduma za ugani zinazohusu:
• Kilimo bora katika mazao yote, lishe, umwagiliaji, matumizi sahihi ya zana za kilimo
• Kilimo cha maghorofani (uzalishaji na ustawishaji wa miche mbalimbali)
• Huduma ya Zahanati ya Afya ya Mimea
3.0. UPATIKANAJI WA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA IDARA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA
Wataalam ngazi ya Manispaa
Katika ngazi ya Makao makuu ya Halmashauri ya Manispaa idara inao watumishi watano (5). Kati yao wanne (4) ni wataalam wenye fani ya Kilimo na Umwagiliaji na mmoja (1) ana fani ya Ushirika. Wajibu wa wataalam hawa katika ngazi hii ni Kuratibu, kusimamia na kufuatilia shughuli zote za kilimo, umwagiliaji na ushirika katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Wataalam hawa wote wanapatikana kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni iliyopo eneo la Kata ya Mjimwema mkabala na Shule ya Msingi ya Mjimwema.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa