KAZI /HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA IDARA YA KILIMO
1.Kutoa ushauri na huduma za ugani kwa wakulima/vikundi vya wakulima kwa kutumia kanuni za kilimo bora.
2.Kuhamasisha na kusimamia uzalishaji wa mazao yanayolimwa katika kata zote
3.Kuratibu shughuli zote za Kilimo
4.Kuhamasisha kuundwa kwa vikundi vya uzalishaji mali vya mazao ya kilimo
5.Kusimamia shughuli na mipango yote inayohusika katika kufikia ufanisi wa mashamba darasa ya vikundi vya wakulima ikiwa ni (kupanga vipaumbele vya mazao, bajeti - pembejeo na shajala, machapisho, kusimamia wahitimu na kushiriki kufanya tathmini ya mafanikio ya mashamba darasa)
6.Kusimamia uibuaji wa miradi ya kilimo kwa njia ya mnyororo wa thamani (value chain)
7.Kusimamia utekelezaji wa miradi ya Kilimo na Umwagiliaji iliyoibuliwa na vikundi vya wakulima
8.Kutoa ushauri katika upatikanaji, utumiaji wa pembejeo za mazao ya kilimo
9.Kutoa ushauri katika usindikaji, utumiaji na upatikanaji wa masoko ya mazao ya wakulima
10.Kufuatilia na kutoa taarifa za mlipuko wa visumbufu vya mimea na maafa mengine yanayoweza kuharibu mazao ya kilimo
11.Kuhamasisha uundaji wa mtandao wa vikundi vya wakulima
12.Kuunganisha vikundi vya wakulima na taasis/ wabia mbalimbali kwa ajili ya kuleta ufanisi katika kilimo na umwagiliaji kwa manufaa ya wakulima
13.Kutafuta mahitaji ya teknologia na taarifa muhimu kwa maendeleo ya kilimo
14.Kutekeleza sera na miongozo mbalimbali inayotolewa kuhusu kilimo na umwagiliaji
15.Kushirikiana na wadau wengine wa kilimo, umwagiliaji kwa ajili ya kuendeleza kilimo
16.Kutoa takwimu zitakazosaidia tafiti endelevu za kilimo na umwagilaji
17.Kuandaa ‘by laws’ za kilimo cha pembezoni mwa mji na kilimo mjini
18.Kuandaa wakulima kwa ajili ya kushindanishwa kwenye maonesho ya wakulima nanenane
19.Kuandaa na kuratibu maonesho ya sikukukuu ya wakulima nanenane
20.Kuweka kumbukumbu sahihi na muhimu zinazohusu masuala ya kilimo na umwagiliaji
21. Kuandaa na kufuatilia takwimu mbalimbali za kilimo na umwagiliaji
22.Kushiriki vikao na mafunzo ya kitaalam
23.Kuandaa taarifa za utekelezaji wa huduma za ugani za kila mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka na kuziwasilisha kwenye ngazi zinazohusika
KITENGO CHA USHIRIKA
Kwa maelezo zaidi soma hapa
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa