Manispaa ya Kigamboni iliundwa kutokana na wilaya mama ya Temeke kupitia Tangazo la Serikali Na. 462 la mwaka 2015 kuhusu mgawanyo wa Wilaya. Wilaya ya Kigamboni ina ukubwa wa kilomita za mraba 416. Aidha, Wilaya ya Kigamboni inapakana na Bahari ya Hindi kwa upande wa mashariki, Wilaya ya Mkuranga upande wa kusini, kaskazini inapakana na Bahari ya Hindi na upande wa magharibi ipo Manispaa ya Temeke
Kufuatia Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Wilaya ya Kigamboni ilikuwa na jumla ya watu 162,932 na kaya 40,133. Kati ya hao wanaume walikuwa 81,199 na wanawake walikuwa 81,733. Wilaya ya Kigamboni ina ongezeko la wakazi linalofikia asilimia 5.6 kwa mwaka hivyo hadi kufikia mwaka huu 2017, Wilaya ya Kigamboni inakisiwa kuwa na watu wapatoa 205,966 na Kaya 48,043. Kati yao wanaume ni 102,645 na wanawake ni 103,321
Ukubwa wa Wilaya Mpya ya Kigamboni na Kuwa na ardhi kubwa ya wazi kuliko Wilaya zote za Jiji la Dar es Salaam, kunaifanya wilaya ya Kigamboni kuwa na fursa nzuri sana katika uwekezaji wa aina zote. hata hivyo Kigamboni kutokana na kuwa na miundombinu ya Uhakika na inayofikika vizuri, inaifanya kuwa sehemu yenye fursa za uwekezaji katika huduma ya Makazi.
Mashirika mbalimbali na wadau wameanza kuzichangamkia hizi fursa za uwekezaji katika makazi wakiwemo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Watumishi Housing company, Avic town na wengine wengi.
Tunapenda kuwakaribisha wadau wa Maendeleo na mashirika mbalimbali kuchangamkia hizi fursa na kuwekeza katika Wilaya yenye ardhi iliyopangwa vizuri kwa matumizi mbalimbali.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa