Katika mpango wa kuhakikisha mji unapangwa kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za mipango miji, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, anawatangazia wananchi kuwa, anauza viwanja zaidi ya 6000 vilivyopimwa vyenye matumizi mbalimbali vikiwemo Viwanda, viwanja hivyo viko katika kata ya Kisarawe II, Somangila, Kimbiji na Pembamnazi.
Fomu za maombi ya kumiliki kiwanja zitauzwa kwa Tshs. 20,000/= katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni
zilizopo Mjimwema.
Idadi ya fomu zitakazouzwa ni sawa na idadi ya viwanja vilivyopimwa.
Waombaji ambao si raia wa Tanzania wanapaswa kupata kibali toka T.I.C
Viwanja vyote vina fikika kwa urahisi. Aidha Barabara zote za ndani ya mradi zimeshafunguliwa na baadhi-
vina miundombinu ya maji na umeme.
Fomu za maombi ya kiwanja zitaanza kutolewa tarehe 18 - 25/04/2017 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 9 alasiri
Fomu hiyo pia unaweza kuipakua hapa ( Fomu ya Maombi ya Kiwanja) na Kuilipia Katika ofisi ya Manispaa baada ya kuijaza
Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 28/04/2017 saa 9 alasiri.
Imetolewa na:
Stephen E. Katemba
MKURUGENZI WA MANISPAA
KIGAMBONI
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa